Back to top

WAZIRI UMMY: SERIKALI KUIPA MTAJI WA BIL. 100, MSD

26 June 2024
Share

Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, amesema Shilingi Bil. 100/= zimetengwa katika mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya kuipatia mtaji Bohari ya Dawa (MSD), ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake.
.
Mhe.Ummy ameyasema hayo leo Juni 26, 2024, Bungeni, Jijini Dodoma wakati akijibu hoja ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Bajeti ya Bunge juu ya Serikali kuiwezesha MSD kwa kuipatia mtaji.
.
Aidha, Waziri Ummy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassani,  kwa kutoa kwa kutoa pesa hizo kwa  mkupuo ili kuimarisha utendaji kazi wa MSD na tayari mabadiliko ya kiutendaji yameanza kuonekana.