Back to top

TCDC YAONYA WANAUSHIRIKA WANAOTOROSHA TUMBAKU

29 June 2024
Share

Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), imewaonya wanaushirika wasio waadilifu, kuacha tabia ya kutorosha zao la tumbaku na kwenda kuuza kwa wanunuzi wengine wasio na mkataba na vyama vyao, hali inayosababisha vyama husika kukosa mapato na kuleta changamoto za ulipaji wa madeni ya mikopo.
.
Onyo hilo limetolewa na Mrajisi wa vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume hiyo, Dkt. Benson Ndiege, wakati akizumgumza na Viongozi pamoja na wanaushirika wa Chama Kikuu cha Ushirika Milambo, kilichopo Tarafa ya Ulyankulu, Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, wakati akiwa ziarani wilayani humo ambapo amewataka wanaushirika hao kila mmoja kuwa mlinzi wa Chama chake kwa kulinda na kufuata taratibu na maelekezo ya Ushirika.
.
Akiwa katika ziara hiyo, pia, Dkt.Ndiege, amezindua ghala la Chama cha Ushirika Mbeta, AMCOS, ambalo limegharimu kiasi cha Shillingi Mil.46/=, fedha zilizotokana na mapato ya ndani ya Chama hicho.