Back to top

Tanzania inahitaji wawekezaji wakubwa kutoka China.

04 September 2018
Share

Waziri Mkuu Mheshimiwa KASSIM MAJALIWA amesema Tanzania inahitaji wawekezaji wakubwa kutoka China ambao watawekeza kwenye viwanda vya mazao ya kilimo, samaki na mifugo.

Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu imesema Mheshimiwa MAJALIWA amesema hayo jijini Beijing alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo wa China, Bwana Han Changfu.

Amesema  katika kipindi hiki ambacho Tanzania imeamua kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda, China ni nchi sahihi kushirikiana nayo kwa sababu ina wawekezaji wa kutosha.

Mheshimiwa MAJALIWA amesema serikali zote mbili ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ziko tayari wakati wowote kuwapokea wawekezaji kutoka China.

Amesema wawekezaji hao watapatiwa ardhi ya kujenga  viwanda ambavyo vitatumia mazao ya kilimo, mifugo na bahari hasa samaki ambayo mengi yanapatikana kwa wingi nchini.