Back to top

Tanzania kutumia mianzi kwa mkaa, kuni na ujenzi ili kuokoa misitu.

28 October 2018
Share


Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya EU na wadau wengine wa Maendeleo imeanzisha mradi wa kuendeleza zao la mianzi ambalo litatumika kwa nishati na ujenzi, ili kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa zaidi ya hekta laki tatu na elfu sabini na mbili za misitu kila mwaka.
 
Mratibu wa Shirika la mianzi Tanzania Donald Kibuti akiongea na wadau wa nishati na uhifadhi wa misitu jijini Dar es salaam amesema katika hatua za awali shirika kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii linandaa mkakati utakaotumika kuhamasisha upandaji wa mianzimiti kwenye mikoa mbalimbali nchini.