Wizara ya Afya imesema kuwa mpaka sasa Tanzania ni salama, na hakuna mtu yoyote aliyepatikana na ugonjwa wa Mpox (awali ulijulikana kama Homa ya Nyani) na bado ugonjwa huo haujaingia nchini .
Kufutatia taarifa rasmi iliyolewa na wizara hiyo, ambayo pia ina jukumu la kufuatilia na kutoa taarifa za mwenendo wa magonjwa, hususani yale ya mlipuko pamoja na tetesi za magonjwa ndani na nje ya nchi, imetoa wito kwa wananchi kushirikiana na serikali kuhakikisha ugonjwa hauingii nchini.
Wizara pia imewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote dhidi ya ugonjwa huo ikiwemo kuepuka kula, kugusa mizoga au wanyama kama vile nyani au swala wa msituni, kugusa majimaji ya mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Mpox.