![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/undpppsite.jpg?itok=praVNeQg)
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) limeeleza kuridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kupambana na ujangili na biashara haramu za nyara unaotekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika mfumo wa ekolojia wa Ruaha – Rungwa.
.
Akizungumza katika kikao cha Kamati Endeshi ya mradi wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya nyara unaofadhiliwa na mfuko wa mazingira duniani Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Shigeki Komatsubara amesema Shirika hilo limeridhishwa na utekelezaji wa mradi huo kwa kuwa unaendeleza utalii na maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania.
.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Abbas Hassan amesema mradi huo ni muhimu sana kwa nchi kwa kuwa unasaidia Wanyama kuendelea kuwepo kutokana na sehemu kubwa ya utalii wa Tanzania unategemea vivutio vya asili wakiwemo Wanyama.
.
Kamati endeshi ya mradi wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya nyara imekutana kwa lengo la kupitia utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2023 na kupitisha bajeti ya mwaka 2024 ambayo itawezesha utekelezaji wa miradi mbadala kwa wananchi na kuendeleza uhifadhi.