![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/chanzooo.jpg?itok=U3y9dx9v)
Tetemeko la ardhi limepiga Dar es salaam majira ya saa mbili na dakika 13 usiku huu na kuibua mshtuko maeneo mbalimbali.
Mtaalam wa Jiolojia kutoka Makao Makuu ya Dodoma Bw. Gabriel Mbogoni amesema tetemeko hilo ni la kiwango cha 5.9 cha kipimo cha ritcher na limetokea Kusini mashariki mwa Dar es salaam na Mkuranga upande wa baharini.
Hakuna madhara yaliyoripotiwa hadi sasa ingawa maeneo ya Pwani, Morogoro, Arusha na Zanzibar wameripoti tetemeko hilo.