![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/tete%202.jpg?itok=UjhF483e)
Zaidi ya watu thelathini wamefariki dunia nchini Indonesia baada ya kutokea tetemeko la ardhi katika moja ya visiwa vya nchi hiyo.
Waokoaji nchini Indonesia, wanaendelea kuwatafuta watu kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka baada ya kutokea kwa tetemeko hilo la ardhi katika kisiwa cha Sulawesi.
Tetemeko hilo lenye ukubwa wa sita nukta mbili kwa kipimo cha richter lilitokea jana asubuhi na kusababisha mamia ya watu kujeruhiwa.
Maelfu ya watu wengine, wamebaki bila makazi baada ya tetemeko hilo kusababisha hasara katika kisiwa hicho.
Kisiwa cha Sulawesi kina historia ya kutokea kwa majanga ya tetemo la ardhi na tsunami na mwaka 2018 zaidi ya elfu mbili walipoteza maisha baada ya majanga hayo mawili.