Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amesema kuna haja ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuziangalia upya gharama za usafirishaji katika bandari ya Mtwara, kwani ni kubwa na hivyo kusababisha meli ya wafanyabiashara kutoka nchini Comoro kusitisha biashara na Tanzania.
Akaongeza kuwa wafanyabiashara wote wataikimbia bandari hiyo lakini pia athari yake ni kubwa kwa uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.