Watu 35 wamefariki Dunia na wengine kadhaa wamejeruhiwa nchini Pakistan baada ya treni za mwendo kasi kugongana.
Msemaji wa kampuni ya reli amesema idadi isiyojulikana ya watu walikuwa bado wamekwama kwenye mabaki ya mabehewa karibu na mji wa Daharki, jimbo la Sindh, na kuongeza kuwa waokoaji wameomba haraka kupelekewa vifaa maalum kuwasaidia kukata vyuma ili kuwatoa.
Afisa mwandamizi wa polisi wa mji wa Daharki, Bwana Umar Tufali amethibitisha idadi ya watu waliofariki Dunia.
Waziri Mkuu wa Pakistan, Bwana Imran Khan amesema ameshtushwa na ajali hiyo na kuahidi uchunguzi kamili kufanyika, Jeshi limetumwa kusaidia juhudi za uoko aji.