Back to top

TVLA IONGEZE KASI UTOAJI HUDUMA KWA WAFUGAJI.

04 August 2024
Share

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,  ameutaka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kuongeza kasi ya uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa wafugaji hasa katika eneo la uchanjaji wa mifugo Vijijini.

Mhe.Senyamule ameyasema hayo alipotembelea Banda la TVLA lililopo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane) yanayoendelea kufanyika katika uwanja wa Nzuguni Jijini Dodoma.

Daktari wa Mifugo Mtafiti wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Isaac Mengele, amesema kuwa TVLA inashiriki Maonesho ya Nanenane kwa lengo la kutoa elimu ya huduma bora za Maabara za Veterinari, kutoa elimu ya utafiti juu ya magonjwa ya wanyama na wadudu waenezao magonjwa hayo pamoja na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya Chanjo za Mifugo kwa wafugaji na wadau wanaotembelea banda la TVLA.

Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) inatoa huduma za uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya Mifugo, Uzalishaji na Usambazaji wa Chanjo za Mifugo, Uhakiki wa ubora wa vyakula vya Mifugo, Usajili na uhakiki wa ubora wa Viuatilifu vya Mifugo, utafiti wa magonjwa ya Wanyama pamoja na huduma ya ushauri na Mafunzo.