Back to top

Uganda yaridhia kutumia bandari kavu ya Isaka kusafirisha mizigo yake.

07 June 2018
Share

Serikali ya Uganda imeridhia kutumia bandari kavu ya Isaka iliyoko katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kusafirisha shehena ya mizigo ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikisafirishwa kwa njia ya barabara kutoka bandari ya Dar-es-Salaam hadi Kampala.

Hali hiyo imetajwa kuwa itarahisisha usafirishaji wa mizigo tofauti na kutumia njia ya barabara kwakuwa bandari hiyo ni kiungo kinachounganisha nchi jirani za Rwanda, Budundi, Uganga, Congo na Sudani ya kusini kupitia ushoroba wa kati wa kibiashara.