Back to top

UHUSIANO TRA, WALIPA KODI WACHANGIA TRIL.5.9 KUKUSANYWA

04 April 2023
Share

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imesema katika kipindi cha robo ya tatu (Januari - Machi) ya mwaka wa fedha 2022/23, imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Tril. 5.9 sawa na 97.9% ya lengo la kukusanya shilingi Tril. 6.0.
.
Mamlaka hiyo imesema moja ya sababu zilizosaidia kufikia kiwango hicho ni kuimarika kwa mahusiano baina ya Mamlaka hyo na walipa kodi ikiwemo utatuzi wa migogoro ya kodi nje ya mahakama.