Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ina upungufu wa vyumba vya madarasa 300 kwa shule za msingi na 20 za sekondari na hivyo juhudi zinahitajika kukamilisha vyumba hivyo ili watoto waweze kusoma katika mazingira mazuri.
Upungufu huo umebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Songea Bi.Tina Sekambo ambapo pia ameeleza jitihada zinazofanyika za kujenga madarasa mapya na kukarabati yaliyochakaa kabla shule hazijafunguliwa
Akikagua ujenzi wa madarasa na ukarabati wa majengo ya shule katika manispaa ya songea mkuu wa mkoa wa ruvuma Bi.Christina Mndeme amesema hataki kusikia wanafunzi wanakosa nafasi kwa visingizio vya upungufu wa madarasa