Ufungaji wa miamba katika Bahari ya Hindi wilayani Kilwa mkoani Lindi , umeongeza uzalishaji wa samaki aina ya Pweza na kufikia tani zaidi ya sitini, kiwango ambacho ni kikubwa ukilinganisha na mkoa wa Mtwara, ambao bado uko chini katika uvuaji wa samaki hao.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Habiba Athumani, wakati wa kutoa elimu ya ufungaji wa miamba, ili kuongeza uzalishaji wa samaki aina ya Pweza.