Back to top

Vyombo vya habari viweke mkakati kuvutia wawekezaji.

25 May 2023
Share

Msemaji mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Gerson Msigwa, amevitaka vyombo vya habari nchini kuwa na mkakati wa kuvutia wawekezaji katika tasnia hiyo ili waweze kukabiliana na changamoto ya uchumi kwa waandishi wa habari.

Msigwa amesema hayo wakati akimwakilisha Naibu Waziri  wa Habari kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya kuzaliwa kwa taasisi ya vyombo vya habari  Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania yanayofanyika Dodoma.
Amesema tasnia ya habari haiwezi kuwa eneo la kuungaunga kwa kila mtu kujikusanya kusanya na kununua vifaa kidogo ikiwemo cable na kamera na kusema ana chombo cha habari.

Aidha Mwenyekiti wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika, MISA Tanzania, Bi. Salome Kitomari ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kwa namna  anavyochukua hatua mbalimbali zilizowezesha waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kuondoa vikwazo vingi katika sekta hiyo.

Amesema MISA  ni taasisi ya vyombo vya habari  Kusini mwa Afrika,ambapo  ina matawi kwenye nchi za Angola,Botswana , Zambia , Malawi, Lesotho,Msumbiji na ambapo tawi la MISA Tanzania ilianzishwa mwaka 1993 kwa jukumu la Uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa habari ukanda wa Kusini mwa Afrika.