Wakazi zaidi ya 3000 waliopo kata za Maramba na Parungu Kasera wilayani Mkinga wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa miundombinu kufuatia kutumia maji ya visima vilivyochimbwa kienyeji hatua ambayo imekuwa ikihatarisha afya zao.
Wakizungumza katika vijiji tofauti vilivyopo kata ya Maramba wilayani Mkinga,viongozi a kamati za maji za vijiji 12 zilizopo katika kata hizo,wamesema kwa upande wa Maramba tanki la kuhifadhia maji lililojengwa miaka zaidi ya 40 iliyopita limechakaa na pia halitoshelezi mahitaji ya idadi ya watu waliokuwepo hivi sasa.
Kwa upande wake mratibu wa kamati za usimamizi wa maji wilayani Mkinga Benadetha Choma amesema wametoa elimu kwa viongozi wa kamati za maji sehemu za vijijini ili kufahamu sera ya maji na jinsi ya kutetea changamoto za huduma hiyo.
Kufuatia hatua hiyo mhandisi wa maji wilayani Mkinga Mhandisi Michael Ndunguru amesema wapo katika mchakato wa kuifanyia ukarabati miundombinu ya maji iliyopo tarafa ya Maramba kwa sababu imechakaa kupita kiasi.