Wakulima wa zao la Ufuta mkoani Lindi wameendelea kufurahia bei ya juu iyojitokeza kwenye mnada ya shilingi elfu 3060 na bei ya chini ikiwa elfu 3020 huku mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirikia, Hassani Yasini Mpako, akiwasisitiza wakulima hao wa wilaya za Liwale, Ruangwa pamoja na Nachingwea kuendelea kusafisha ufuta wao na kisha kuupeleka kwenye vyama vya msingi na wasikubali kuwauzia walanguzi wasubiri kuuza kwa njia ya mnada tu ambayo ina manufaa makubwa kwao na familia zao.
Wakizungmza na ITV katika kijiji cha Kibutuka wilaya ya Liwale ulikofanyika mnada wamewashukuru viongozi wa chama kikuu cha ushirika cha Runali kwa kuendelea kuwasimamia na kuwapa elimu ya kutouza ufuta wao kwa bei ya chini kwa walanguzi.