![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/IMG-20230505-WA0092-1024x683.jpg?itok=3ba_kO81)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. Deogratius Ndejembi, amesema serikali imewachukulia hatua watumishi wote, waliopatikana na hatia ya kuchezea na kuzima mashine za kukusanyia mapato katika halmashauri za (POS ) na kusababisha upotevu wa mapato katika halmashauri hizo.
Amesema hayo bungeni Dodoma, akijibu swali ambapo amesema kwa sasa pia serikali imefanya maboresho ya mfumo mpya wa "TAUSI" ambao katika halmashauri zote mkurugenzi ana uwezo wa kuona mapato yote yanayokusanywa kwa wakati huo au endapo mashine itakuwa imezimwa.