Wananchi Mkoani Kigoma wameilalamikia serikali kwa kutoa amri ya kuwaondosha katika eneo lililopo karibu na uwanja wa ndege ambapo walikuwa wakiendesha shughuli za kilimo. Wananchi hao wamedai kuwa wamemiliki mashamba hayo kihalali kwa muda mrefu.
Kwa upande wake meneja wa uwanja wa ndege Kigoma Theophany Bileha amesema shughuli zinazofanywa pembezoni mwa uwanja huo zinaathiri maendeleo ya uwanja huo na zinaweza kuleta athari wakati wa kutua au kupaa kwa ndege .
Licha ya malalamiko hayo kutoka kwa wananchi, Naibu waziri wa mawasiliano na uchukuzi Mh.Atashasta Nditie ameagiza kuondolewa kwa watu wote waliovamia maeneo hayo pamoja na mazao yaliyolimwa katika maeneo hayo