Back to top

Wananchi kijiji cha Ifinga Madaba waomba kupatiwa mawasiliano ya simu

14 July 2018
Share

Wananchi wa kijiji cha Ifinga  katika halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma hawana mawasiliano ya simu hivyo kuwalazimu kutumia shilingi  15,000  kwa usafiri wa Pikipiki kwenda eneo pekee lenye mtandao kupiga simu.

Wakiongea na ITV katika kijiji cha Ifinga wanasema kuwa  mambo mengi yamekuwa yakikwama kutokana na kukosekana kwa mawasiliano ya simu na hivyo wanaiomba serikali kwa kushirikiana na makampuni ya simu kutatua changamoto hiyo.

Kwa upande wao walimu katika kijiji cha Ifinga wanasema kuwa wamekuwa wakitumia gharama kubwa kufuatilia mishahara kutokana na kukosekana mawasiliano.