Back to top

Wananchi Lupembe mkoani Njombe walalamikia ukosefu wa minara ya simu.

04 January 2019
Share

Baadhi ya wananchi wa kata za Mfiriga,Idamba,Ninga ,Ikondo ,na Ukalawa zilizopo tarafa ya Lupembe wilaya ya Njombe mkoani Njombe wamemlalamikia naibu waziri wa ujenzi na mawasiliano Mhe.Elias Kwandikwa juu ya ukosefu wa minara ya mawasiliano  kwa ajili ya simu za viganjani kwa muda mrefu sasa,jambo ambalo limekuwa likiwaathiri katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Aidha kufuatia kilio hicho,wakazi hawa pia wanakabiiliwa na changamoto ya ubovu wa barabara hususani wakati wa masika,jambo ambalo wanaiomba serikali kuwajengea barabara kwa kiwango cha Lami,kilio ambacho kinaungwa mkono na mbunge wa jimbo la Lupembe mkoani Njombe Mhe.Joram Hongoli.

Kutokana na malalamiko hayo,inamlazimu naibu waziri wa ujenzi na mawasiliano Mhe.Elias Kwandikwa kujitokeza mbele ya wananchi na kutosa kauli ya serikali ambayo inaleta matumaini mapya kwa wananchi hawa.

Kero ya ukosefu wa minara ya mawasiliano ya simu na ukosefu wa miundombinu bora ya barabara kutoka makao makuu ya mkoa huu wa Njombe mpaka tarafa ya Lupembe imedaiwa kuwa chanzo cha kukwamishwa kwa maendeleo ya wakazi hao licha ya eneo la Lupembe kuwa vinara wa uzalishaji wa mazao ya chai,mbao,viazi mviringo na parachichi.