Back to top

Wananchi mkoani Ruvuma wametakiwa kujitolea kuchangia damu

31 March 2019
Share

Wananchi mkoani Ruvuma wametakiwa kujitolea kuchangia damu kwa kuwa matumizi ya damu mkoani humo ni makubwa wakati hamasa ya wananchi kuchangia damu ni ndogo ukilinganisha na mahitaji hospitalini.

Wito huo umetolewa na kiongozi wa timu ya damu salama mkoani Ruvuma Bw.Imani Mohamed toka hospitali ya mkoa wa Ruvuma wakati akizungumza kwenye zoezi la kuchangia damu lililofanyika kwenye msikiti wa jumuiya ya waislamu wa Ahmadiyya Songea ambapo waumini wa jumuiya hiyo wamejitolea kuchangia damu katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma.

Wakizunguzungumza na ITV waumini wa jumuiya ya waislamu wa Ahmaddiya waliojitolea kuchangia damu kutokana na umuhimu wa damu hospitalini