Back to top

WANANCHI WA VISIWA VYA COMORO KUTIBIWA BMH

03 September 2024
Share

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe.Moustadroine Abdou, amesema wananchi wa Comoro hawana haja ya kusafiri mpaka Ulaya na Mashariki ya Mbali kufuata huduma za Afya, kwani sasa watatibiwa nchini Tanzania.  

Mhe.Moustadroine Abdou, ameeleza haya alipotembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), nakueleza kuwa huduma walizokuwa wanazifuata Ulaya na Asia, kama kama upandikizaji wa figo, huduma hizo wanaweza kuzipata nchini Tanzania

Mhe.Spika wa Visiwa vya Comoro Mhe.Moustadroine, pia ametembelea idara za Magonjwa ya Moyo, Huduma ya Upandikizaji Uloto (Tiba ya Sikoseli), Idara ya Radiolojia (MRI), Kliniki maalumu ya Viongozi na Wodi ya Rais katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Afya, Dkt Godwin Mollel, amesema ziara hiyo imempa fursa Mhe. Spika wa Bunge wa Visiwa vya Comoro kushuhudia mageuzi makubwa aliyoyafanya Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Afya.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dkt. Kessy Shija, amesema BMH inahudumia zaidi ya wananchi milioni 14 katika Kanda ya Kati na mikoa ya jirani.

Dkt. Shija ameongeza katika ushirikiano huu wa BMH na Visiwa vya Comoro, Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) itafanya huduma mkoba (medical outreach) katika Visiwa hivyo vilivyopo Kusini Mashariki ya Afrika.