Back to top

Wananchi walalamikia kutozwa fedha vitambulisho vya Taifa Kigoma

09 May 2018
Share

Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA ofisi ya Kigoma imelazimika kubadili utaratibu wa kupata baadhi ya nyaraka baada ya wananchi kulalamika kutozwa kiasi cha shilingi elfu tano kwa ajili ya kiapo cha kuzaliwa hali ambayo imesababisha usumbufu kwa wananchi.

Afisa wa NIDA mkoani Kigoma Miriam Buyekwa amesema hayo baada ya kusikia malalamiko ya wananchi, kuwa wamesitisha utaratibu huo ambao uliwekwa na wenyeviti wa mitaa ili kurahisisha upatikanaji wa viapo na kwamba sasa kila mwananchi atalazimika kujaza fomu maalum ya kuthibitisha taarifa zake.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga amesema baada ya kutembelea vituo vya kujiandikisha katika kata za mwanga kaskazini na Mwanga Kusini ambapo amesema zoezi hilo ni bure na hatakiwi mwananchi kutozwa fedha na kwamba tahadhari zimechukuliwa ili wahamiaji na wageni wasipate vitambulisho.