Back to top

Wananchi walalamikia semu yao ya ardhi kupewa muwekezaji Kilombero.

22 March 2019
Share

Wananchi wa Tarafa ya Mngeta, Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro wanaotegemea kilimo kuendesha maisha yao, wamelalamikia sehemu kubwa ya ardhi waliyonayo kupewa mwekezaji mkubwa hivyo kukosa maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo.

Wakulima hao wamesema hayo wakati wa kongamano la kujadili matatizo yanayomkabili mkulima mdogo, hasa mwanamke, lililoandaliwa na mtandao wa vikundi vya  wakulima (MVIWATA) na kufanyika Kijijini Mngeta.

Kongamano hilo limekwenda pamoja na shughuli za utoaji msaada wa sheria kwa wakulima wadogo waliopoteza haki za kumiliki ardhi ambapo wakabainisha maeneo mengi yaliyopewa wawekezaji wakubwa, wengine wameshindwa kuyaendeleza.

Katika kongamano hilo ambalo wakulima zaidi ya 100 walijitokeza kutaka msaada wa sheria wa migogoro yao mbalimbali ya ardhi, baadhi yao pia wakalalamikia riba kubwa inayotozwa na taasisi mbalimbali za fedha kuwa zimeendelea kudumaza maendeleo ys mkulima mdogo.