Back to top

'Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi kutengewa bajeti'

25 October 2018
Share

Serikali imeziagiza halmashauri zote nchini kutenga bajeti kwa ajili ya kuwahudumia watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi na kwamba inaendelea na mikakati ya kuboresha utoaji huduma katika sekta ya afya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Suleiman Jafo ameagiza halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongowazi. 

Ametoa agizo hilo jijini Dodoma akifungua maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya mtoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi.

Aidha, amewataka wazazi na walezi kuondokana na imani potofu za kishirikina kuhusu vyanzo vya magonjwa hayo na wawapelele watoto wao hospitali kwani yanatibika.

Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi Wenye Watoto wenye Vichwa Vikubwa na Mgongo Wazi Tanzania, Bwana. Abdulhakim Bayakub  amesema idadi kubwa ya Watanzania hawana elimu juu ya kinga ya tatizo hilo, hivyo ameiomba serikali kuendelea kuwahamasisha wazazi wasiwafiche watoto wenye matatizo hayo.