![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/ugali.jpg?itok=OEDdPdJj)
Watu wawili wamefariki dunia kati ya watu ishirini na tano wa familia tofauti waliosadikiwa kula chakula chenye sumu katika kijiji cha Busumba kata ya Bwiro wilayani Ukerewe mkoani Mwanza walichokinunua kutoka kwa wafanyabiashara wanaoingiza chakula kutoka mikoa mbali mbali kutokana na upungufu wa chakula.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Cornel Maghembe ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo amebainisha baada ya madiwani kuibua hoja upungufu wa chakula katika baraza maalumu la madiwani la kutathimini hali ya makusanyo ya fedha katika robo ya kwanza ya mwaka chakula na mazingira kwa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe
Kaimu afisa kilimo wa wilaya hiyo Issa Ibrahimu amesema kutokana na hali hiyo wameanza mikakati ya kutoa elimu kwa wananchi kulima kilimo cha tija na mazao yanayoendana na hali ya sasa ya mvua huku mbunge wa Ukerewe akiomba serikali kuona namna ya kutoa chakula cha bei nafuu hili kiweze kusaidia katika kipindi hiki.
Akifunga baraza hilo la siku mbili mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mhe.George Nyamaha amewataka viongozi wa serikali kuacha tabia ya kutosema ukweli kuhusu uwepo wa hali ya upungufu wa chakula wilayani hapo kwani hali hiyo inasababisha wananchi kuishi maisha ya tabu huku serikali inauwezo wa kuwapatia chakula cha bei nafuu.