Back to top

Wawekezaji katika sekta ya madini watakiwa kutumia vizuri fursa.

15 May 2019
Share

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Bwana.Godfrey Simbeye amewataka wawekezaji katika sekta ya madini kutumia vizuri fursa waliyopata ya kukutana na wawekezaji kutoka china ikiwa ni pamoja na kujenga mtandao wa kuwawezesha kushirikiana katika uchimbaji, na uchakataji wa rasilimali hiyo.Bwana.Simbeye ameyasema hayo katika kikao chao na wawekezaji kutoka china ambao ni sehemu ya watalii zaidi ya 300 walioko nchini kutembelea vivutio katika hifadhi za taifa.Kwa upande wake waziri wa uwekezaji MheAngella kairuki amesema fursa za uwekezaji zilizopo nchini Nyingi na wawekezaji bado wanahitajika na serikali inaendelea kuboresha mazingira yakuwawezesha wadau kuwekeza.Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Waziri wa vijana Bwana.Anthony Mavunde amesema fursa zinazoendelea kujitokeza zikitumika vizuri licha kupunguza tatizo la ajira itaharakisha kufikiwa ukuaji wa uchumi. Rais wa shirikisho la vyama vya wachimbaji Madini Tanzania John Bina amesema wawekezaji kutoka china wameonyesha nia ya kuwekeza katika sekta hiyo hatua ambayo ikifikiwa itaongeza tija na  pato kwa wannchi na taaifa kwa ujumla.