Back to top

WODI 128 WATOTO NJITI ZAJENGWA, NYINGINE 100 KUONGEZWA.

12 October 2023
Share

Serikali imesema imejenga wodi maalumu za uangalizi wa watoto njiti 128, huku ikibainisha kuwa ,kwa mwaka huu 2023, imepanga kujenga wodi zingine 100, ili kuhakikisha vifo vya watoto wachanga vinapungua au kuisha kabisa.
.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, wakati akifungua mkutano wa 24 wa Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania, unaofanyika Jijini Dodoma, ukiwa na lengo la kuangalia ustawi wa mtoto kuanzia anapozaliwa mpaka kukua kwake.

Aidha, Naibu Waziri huyo, amewataka Madaktari Bingwa wa Watoto nchini, kuendelea kuwahudumia vizuri watoto wanaozaliwa kabla ya siku na wale wanaozaliwa kawaida kwani wote wanahitaji uangalizi wa karibu katika ukuaji wote.