Wakulima wa ukanda wa Tambarare wa wilaya za Same, Mwanga, Moshi na hai wameshauriwa kulifanya zao la fiwi kuwa zao kuu la biashara baada ya utafiti kuonyesha linastamili ukame na gharama ndogo za uzalishaji ikilinganishwa na mazao mengine.
Akiwakilisha taarifa yake ya utafiti kwa maafisa kilimo wa kata, madiwani na viongozi wa dini wa wilaya ya Same mtafiti mwandamizi wa mazao yanayovumilia ukame na mbegu bora nchini Dkt. Mary Mgonja amesema, utafiti wa majaribio aliyoufanya kuanzia mwaka 1993 umeleta mabadiliko makubwa ya maisha ya wananchi wa kijiji cha mabilioni wilayani Same.