
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa anaamini kushindwa kufanikiwa kwa mazungumzo ya kumaliza uvamizi wa Urusi kutamaanisha "vita ya tatu ya dunia" ambapo akizungumza na CNN Zelensky alisema yuko tayari kuzungumza moja kwa moja na Rais wa Urusi Vladimir Putin huku akiongeza kuwa anaamini kuwa mazungumzo ndiyo njia pekee ya kumaliza mapigano.