Back to top

ZIARA YA RAIS SAMIA MAREKANI YATAJWA KUZAA MATUNDA

26 October 2022
Share

Ziara ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan nchini Marekani inatajwa kuzaa matunda Mara baada ya ujumbe wa wawekezaji 35 kutoka Marekani kufika nchini kuja Tanzania kutazama fursa za uwekezaji Katika maeneo mbalimbali.

Ziara hiyo inatajwa kuwa ya kimkakati ikilenga uwekezaji Katika viwanda, utalii na sekta ya Kilimo ambapo sasa wawekezaji hao wamekutana na wadau wa Ndani kutazama Kwa namna gani wao wanaweza kuweka mitaji yao nchini.

Hata hivyo Kwa tafiti za umoja wa mataifa Tanzania inatajwa kati ya nchi 10 Afrika ikishika nafasi ya tisa Kwa kuvutia Uwekezaji.

Kwa muda mrefu wafanyabiashara wengi wa Tanzania wamekuwa wakilalamikia changamoto ya upatikanaji wa mitaji hivyo kupitia ziara hizi sasa zinafungua fursa za uwekezaji Kwa wazawa ambapo wawekezaji hao wamesema wamehamasika na mwenendo na Kasi ya uwekezaji Tanzania.