Back to top

"WAZAZI JENGENI UKARIBU NA WATOTO WENU"

13 February 2024
Share

Polisi Kata Manispaa ya Morogoro, limewasihi wazazi na walezi kujenga ukaribu na watoto wao ili kufuatilia nyendo zao, hasa kwa wale wanaosoma, baada ya kubainika kuwepo kwa wanafunzi watoro shuleni ambao wamekutwa wakiwa wamejichanganya na makundi hatarishi.

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kata ya Mkundi Wilayani Morogoro A/INSP Anna Manumbu, ametoa wito huo baada ya kubaini baadhi ya wanafunzi wa shule ya Mkundi-Mguluwandege, kata Mkundi Mkoani Morogoro, ambao wamekuwa watoro shuleni hapo na kujificha vichakani wakiwa na makundi hatarishi, ambapo katika kuwafatilia wameweza kuwapata na kuwarudisha shule ya Mkundi kuendelea na masomo.

Kadhalika A/INSP Anna Manumbu, amewataka walimu kuhakikisha panapojitokeza sintofahamu kama hiyo wanatoa taarifa kwa polisi Kata katika eneo husika ili kudhibiti hali hiyo, kwani wanafunzi hao wakijengewa misingi imara ndio viongozi wa baadae katika Taifa la Tanzania.