Back to top

TVLA YAPONGEZWA UTOAJI ELIMU YA MIFUGO

10 July 2024
Share

Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), umepongezwa kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya uchunguzi wa magonjwa ya wanyama na uchanjaji wa mifugo, ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali iliyopo Mkoa wa Mbeya, Bw. Missana Kwangura baada ya kutembelea banda la TVLA, kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es salaam (Sabasaba).

TVLA ni wakala unaohusika na uchunguzi wa magonjwa ya wanyama, uzalishaji na usambazaji wa Chanjo za Mifugo, utafiti wa magonjwa ya wanyama na wadudu waenezao magonjwa hayo pamoja na uhakiki wa ubora wa vyakula vya Mifugo.