Back to top

DUGANGE AIPONGEZA 'CALL CENTER' WIZARA YA KILIMO

04 August 2024
Share

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI – Afya) ametoa  wito kwa Wizara kuendelea kuitangaza namba ya kituo cha huduma kwa wateja ambayo ni 0800110810 au 0733800200 ili iweze kuwafikia wakulima wote nchini kuitumia namba hiyo kama fursa kupata huduma kutoka kwa wataalam wa kilimo.


Naibu Waziri ametoa wito huo alipotembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa NaneNane ikiwemo banda la Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Wizara ya Kilimo na kuishauri Wizara kuendelea kuboresha huduma ya kituo cha huduma kwa wateja na ikiwezekana kuanzisha vituo vingine ngazi ya Mkoa ata Wilaya.