Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 120 katika shule tano za msingi wilayani ya Kibiti, na Mabati 145 kwa ajili ya kuezekea majengo kwenye shule ya Sekondari ya Mahoro, iliyopo wilayani Rufuji mkoani Pwani.
Akipokea msaada huo Mkuu wa wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo, amesema sekta zilizopewa kipaumbele na benki ya NMB katika kurejesha kwa jamii, sehemu ya faida wanayopata kila mwaka, ni sekta ambazo serikali imezipa kipaumbele kwenye ajenda zake.
Kwa upande wao Benki ya NMB, kupitia Meneja wa Kanda ya Dar es salaam na Pwani, Seka Urio amesema suala la uboreshaji wa elimu nchini, ni ajenda iliyopewa kipaumbele ndani ya benki hiyo, na kwamba kila mwaka wanatenga asilimia moja ya faida wanayopata baada ya kodi, kurejesha kwa jamii ikiwamo sekta elimu, afya, mazingira na majanga