Back to top

TAWIRI YAPONGEZWA SHUGHULI ZA UTAFITI WANYAMAPORI

22 October 2024
Share

Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kwa shughuli za utafiti wa Wanyamapori ambazo zina tija katika  sekta ya uhifadhi na utalii  ambayo inachangia asilimia 17% ya pato la Taifa.

Akizungumza jijini Arusha wakati wa kikao na Menejimenti ya TAWIRI, Bw. Mchechu amesema Ofisi ya msajili wa Hazina  itaendelea kushauri vyema katika kuimarisha Mashirika ya Umma yaweze kujiendesha kwa tija.
 
“Nawapongeza kwa utendaji mzuri, nitoe wito kuendelea kuwa wabunifu kutumia  rasimali mlizonazo kujiendesha kwa ufanisi,” amehimiza Bw.Mchechu.

Naye, Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dk. Eblate Mjingo, amesema TAWIRI ni taasisi ya kimkakati ambayo mbali na kutokuonekana ikizalisha fedha moja kwa moja ina mchango  mkubwa katika mapato yatokanayo na utalii nchini ambapo takwimu na taarifa za tafiti ndizo zinazonadi utalii na kuimarisha uhifadhi.