Back to top

UTEKELEZAJI MKATABA HAKI ZA WANAWAKE BARANI AFRIKA

22 October 2024
Share

Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Idara ya Haki za Binadamu imewakutanisha wadau mbalimbali kutoka Bara na Zanzibar katika kikao kazi cha kukamilisha taarifa ya Nchi ya kufuatilia utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu pamoja na Mkataba wa Haki za Wanawake barani Afrika (Itifaki ya Maputo). 

Katika kikao hicho kitaandaa taarifa itakayoonesha ni kwa namna gani kwa mujibu wa Mikataba Haki za Wanawake barani Afrika (Itifaki ya Maputo), katika Nchi ya Tanzania, ni kwa namna gani imefanikiwa kutekeleza viwango ambavyo Nchi inapaswa kuvifuata katika kuendeleza na Kulinda Haki za Wanawake.

Itifaki ya Maputo imekuwa na manufaa makubwa katika kuwezesha na kuendeleza upatikanaji wa Haki pamoja na kuonesha jitihada zinazofanywa na Serikali katika kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya  Wanawake nchini Tanzania.