Back to top

'KIDONGE' CHA KUZUIA UVUTAJI SIGARA KUTOLEWA UINGEREZA

12 November 2024
Share

#HABARI: Uingereza imetangaza kuanza kutoa  kidonge maalumu kijulikanacho kama 'Varenicline' kwa wavutaji sigara nchini humo, ambao wako tayari kuacha kuvuta sigara.

Kidonge hicho cha Varenicline ambacho kimetajwa kuwa mbadala kwa wavutaji sigara wenye nia ya kuachana kabisa na matumizi ya sigara, kinasemekana kupunguza tamaa na athari za nikotini ambazo huwafanya watu kuwa warahibu.

Kidonge hicho pia husaidia kupunguza changamoto wanazopitia wanaotaka kuachana na urahibu huo, kama vile kuwashwa au shida za kulala, ambazo kwa kawaida huchukua hadi wiki 12.

Varenicline itakuwa chaguo jingine kwa watu wanaotumia huduma za NHS, kuacha kuvuta sigara nchini Uingereza.

Walakini, NHS ilisema toleo la jumla la dawa hiyo, kutoka kwa kampuni ya dawa ya Teva UK, sasa imeidhinishwa kuwa salama na Mamlaka ya Afya na Udhibiti wa Dawa (MHRA).