Back to top

RIPOTI YA UCHUMI WA DUNIA, UCHUMI WA TANZANIA UNAKUA

17 December 2024
Share

Ripoti ya Fitch Ratings umeipa Tanzania kiwango cha alama B+ kuwa na Uchumi unaokua kwa kasi na uwezo wa Kulipa Madeni ya Nje kwa Muda Mrefu (IDR).

Ripoti hiyo imeonyesha mtazamo thabiti wa mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Sera nzuri za kifedha na kiuchumi za serikali ya Rais Samia zimeiongoza nchi kuelekea ustahimilivu na ukuaji, hata katikati ya changamoto za kiuchumi duniani.

Kuimarisha Ukuaji wa Kiuchumi Chini ya uongozi wa Rais Samia, ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) wa Tanzania unatarajiwa kufikia asilimia 5.4 mwaka 2024 na asilimia 5.9 mwaka 2025, ukipita wastani wa nchi nyingine zenye alama sawa.

Mafanikio haya ni matokeo ya moja kwa moja ya uwekezaji wa kimkakati wa serikali yake katika miradi ya miundombinu yenye mabadiliko makubwa, kama vile Reli ya Kisasa (SGR) na Mradi wa Umeme wa Bwawa la Julius Nyerere.

Miradi hii inaonyesha dhamira ya rais ya kuboresha uchumi, kuunda nafasi za ajira, na kuhakikisha maendeleo endelevu.

Msisitizo wa Rais Samia katika kufufua sekta muhimu kama kilimo, madini, na utalii umechangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarika kwa uchumi wa Tanzania.

Msaada wa serikali yake kwa miradi mikubwa si tu umevutia uwekezaji wa kigeni bali pia umefungua uwezo wa muda mrefu wa ukuaji wa nchi.

Kudhibiti Mfumuko wa Bei na Kustawisha Uchumi, Serikali ya Rais Samia imefanikiwa kudumisha mfumuko wa bei chini ya lengo la asilimia 5 la Benki Kuu ya Tanzania, kwa wastani wa asilimia 3.1 katika robo ya tatu ya mwaka 2024.

Mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za serikali kuhakikisha usalama wa chakula kupitia sera bora za kilimo na usambazaji wa pembejeo kwa ufanisi.

Mabadiliko ya mfumo wa sera za kifedha kuelekea matumizi ya viwango vya riba kama kipimo kikuu ni hatua nyingine muhimu, ambayo imeimarisha ufanisi wa sera za Benki Kuu. 

Mageuzi haya yanaonyesha dhamira ya serikali ya Rais Samia ya kudumisha uthabiti wa kiuchumi na kuimarisha imani ya wawekezaji.