Back to top

MALI ZA USHIRIKA ZIWEKEZWE KWA TIJA- DK. NINDI

09 March 2025
Share

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Ushirika & Umwagiliaji- Dkt.Stephen Nindi amevitaka vyama vya Ushirika kuwekeza Mali za Ushirika kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Ushirika ili kuleta tija na manufaa kwa Wanaushirika na jamii kwa ujumla.

Amebainisha hayo wakati alipotembelea  miradi ya uwekezaji ya Vyama vya Ushirika katika ziara yake ya kikazi Machi 7, 2025 Mkoani Kilimanjaro.

Amesema ni muhimu Viongozi wazingatie na kutekeleza Mikataba wanayoingia na wawekezaji kwa maslahi ya Vyama ili kuepusha migogoro na kuongeza tija kiuchumi.

Maeneo ya Miradi aliyotembelea Mkoani Kilimanjaro ni pamoja na Mashamba ya Uwekezaji  Lambo, Mulomo, Lerongo,  Mradi wa pamoja Fonrwa pamoja na Kampuni ya Kilimo na uchakataji wa Parachichi Africado.

Viongozi mbalimbali wameshiriki Ziara hiyo  akiwemo Naibu Mrajis - Udhibiti Collins Nyakunga pamoja na watendaji  wa Taasisi mbalimbali kwa lengo na kujifunza na kupokea maelekezo ya kuongeza tija kwenye Ushirika.