
Katika kilele cha siku ya wanawake dunia Mkoa wa Singida, imeunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kupambana na matumizi ya nishati chafu na kuhamia kwenye nishati safi, kwa kutowa mitungi zaidi ya 29,000 kwa wanawake wa Mkoa wa Singida kwa bei nafuu ambayo ita zinufaisha kaya 350,000 za mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi. Halima Dendego, amesema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake kimkoa, ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na kudai kuwa mitungi hiyo itawasaidia wanawake hasa wa vijiji kuboresha afya zao ambazo zilikuwa zikiathirika na moshi wa kuni.
Kwaupande wao baadhi ya wanawake walio patiwa mitungi hiyo wamesema matumizi ya gesi yatawasaidi kuondokana na magonjwa yatokananyo na moshi, huku Afisa wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida, Rahma Abdarabi, ametoa mafunzi ya kwa namna gani moto unaosababishwa na gesi unadhibitiwa ilikujikinga na kutumia mitungi kwa uagalifu kwa kuhakikisha mtungi unazimwa kila unapo maliza matumizi
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dk. Fatuma Mganga, amesema mkoa umefanya shughuli za matendo ya uhuruma kwa kutowa misaada mbalimbali kwa wenye mahitaji na wanawake walio lazwa kwenye hospita mbalimbali.
Maadhimisho yameenda pamoja na maandamano maonyesho mbalimbali ikiwemo shughili zinazo fanywa na wanawake za ulinzi , kuendesha mitambo mikubwa ya ujenzi na jinsi ya kuzima moto.