Back to top

Gesi asilia yaanza kusambazwa majumbani.

20 May 2018
Share

Waziri wa Nishati Dkt.Merdad Kalemani amesisitiza matumizi ya Gesi asilia ambayo imeanza kusambazwa majumbani ikiwa ni mpango mahususi wa serikali wa  kupunguza matumizi ya Mkaa ambayo yamechangia kwa kiasi kikubwa  uharibufu wa mazingira ikiwemo uchomaji holela misitu na kuzalisha mkaa katika maeneo mbalimbali hapa.


Dkt. Kaleman ametoa msisitizo huo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua mpango wa matumizi ya Gesi asilia majumbani inayozalishwa na serikali na kusimamiwa na shirika la maendeleo ya Pertoli nchini TPDC itayoanza kusambaza kiwango cha Gesi zenye futi za ujazo trilioni 1.2 kwa kuanzia mikoa ya Dar es Salaam,Lindi na Mtwara ikiwa ni mpango mahususi wa serikali wa kupunguza matumizi ya mkaa majumbani.

Akitoa taarifa juu ya mradi huo ikiwa ni sehemu ya awamu kwanza ya usambazaji wa gesi hiyo majumbani mtendaji mkuu wa TPDC,Mhandisi Kapuulya Musomba amesema mradi huo umegharimu shilingi bilioni 4 ukitoa fursa kwa maandalizi ya awamu ya pili  utakaogharimu shilingi bilioni 11 huku mkuu wa wilaya ya Ubungo Kisare Makori akiwahimiza wananchi kutumia gesi asilia kwa sasa kutokana na idadi kubwa ya wananchi bado wanatumia nishati ya mkaa.

Baadhi ya wananchi ambao mradi wa bomba umepita karibu na nyumba zao wakiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi wa gesi wakaiomba serikali kuwalipa fidia zao kwa wakati ili kupisha haraka mabomba ya Gesi.