
Waziri wa maliasili na utalii Mhe.Dkt Khamis Kigwangallah amewasilisha bajeti ya wizara yake na kubainisha changamoto zinazoikabili wizara hiyo ikiwemo Ujangili na biashara haramu ya nyara za serikali .
Mhe.Kigwangallah amesema licha ya kufikia kwa mafanikio makubwa katika wizara hiyo lakini zipo changamoto ambazo kimsingi nazo zinawaongezea ugumu wa kazi.
Kwa upande wake waziri kivuli wa wizara hiyo Mhe.Peter Msigwa na ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi maliasili na utalii amesema wizara imeshindwa kuwalinda wawekezaji kutokana na matamko mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa na wizara.
Naye mwenyekiti wa kamati ya kudumu inayohusika na wizara hiyo amesema serkali inapaswa kutenga fedha za kutoka katika wizara hiyo huku baadhi ya wabunge wakitoa maoni yao kuhusu bajeti hiyo.