Back to top

Wakulima wa zao la Ufuta wafurahishwa na bei nzuri kwenye mnada

11 July 2018
Share

Wakulima wa zao la Ufuta mkoani Lindi wameendelea kufurahia bei ya juu iyojitokeza kwenye mnada ya shilingi elfu 3060 na bei ya chini ikiwa elfu 3020 huku mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirikia, Hassani Yasini Mpako, akiwasisitiza  wakulima hao wa wilaya za Liwale, Ruangwa pamoja na Nachingwea kuendelea kusafisha ufuta wao na kisha kuupeleka kwenye vyama  vya  msingi na wasikubali kuwauzia walanguzi wasubiri kuuza kwa njia  ya mnada tu ambayo ina manufaa  makubwa kwao na familia zao. 

Wakizungmza na ITV katika kijiji cha Kibutuka wilaya ya Liwale ulikofanyika mnada wamewashukuru viongozi wa chama kikuu cha ushirika cha Runali kwa kuendelea kuwasimamia na kuwapa elimu ya kutouza ufuta wao kwa bei ya chini kwa walanguzi.