Wananchi wa kijiji cha Ifinga katika halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma hawana mawasiliano ya simu hivyo kuwalazimu kutumia shilingi 15,000 kwa usafiri wa Pikipiki kwenda eneo pekee lenye mtandao kupiga simu.
Wakiongea na ITV katika kijiji cha Ifinga wanasema kuwa mambo mengi yamekuwa yakikwama kutokana na kukosekana kwa mawasiliano ya simu na hivyo wanaiomba serikali kwa kushirikiana na makampuni ya simu kutatua changamoto hiyo.
Kwa upande wao walimu katika kijiji cha Ifinga wanasema kuwa wamekuwa wakitumia gharama kubwa kufuatilia mishahara kutokana na kukosekana mawasiliano.