Back to top

Tetemeko la ardhi laua watu zaidi ya 1,234 Indonesia.

02 October 2018
Share

Watu zaidi ya 1,234 wamepoteza maisha nchini Indonesia kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo mwishoni mwa wiki.

Inaelezwa katika mji wa Palu pekee jumla ya watu 840 na arobaini wamepoteza masiha mpaka sas na kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Maafa hayo yaliyosababishwa na Tsunami mpaka sasa yamejeruhi watu zaidi ya 799 ambapo taarifa zaidi zinasema mapema leo tetemeko lingine limetokea katika Kisiwa cha Sumba kilichopo Mashariki mwa Indonesia na sehemu ya eneo la Palu.