Back to top

Mkuu wa chuo cha ualimu Shinyanga Shycom atumbuliwa

06 October 2018
Share

Mkuu wa chuo cha ualimu Shinyanga SYCOM Bw.Paschal Highmagway ametumbuliwa kwa kosa la kutoa taarifa ya uongo mbele ya waziri wa elimu,sayansi teknolojia na ufundi Mhe.Joyce Ndalichako na kumsifia mkandarasi anayejenga mabeni ya chuo kinyume na muonekano wa kazi hiyo inayoonekana tofauti na taarifa yake.

Waziri wa elimu Mhe.Joyce Ndalichako ametoa kauli ya kumsimamisha kazi mkuu wa chuo hicho na kumuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kumuondoa mara moja katika nafasi yake mkuu wa chuo Bw.Pascal Highmagway baada ya kupokea taarifa yenye sifa kede kede inayomsifia mkandarasi anayejulikana kwa jina la Thadeus Koyanga kutoka katika kampuni ya Afriqengeneering ya Jijini Dar es Salaam tofauti na hali aliyoiona baada ya kukagua ujenzi hali ambayo imemchukiza na kudai kuwa hawezi kupokea taarifa ya uongo na kuinyamazia.