Back to top

Marufuku vifaa vya ujenzi majengo wa serikali kutoka nje.

18 November 2018
Share

Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe.Selemani Jaffo amepiga  marufuku uagizaji wa vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 350 na hospitali za wilaya zinazoendelea kujengwa ili zaidi ya shilingi bilioni 105 ambazo serikali inatarajia kuzitumia mwaka huu katika ukamilishaji wa ujenzi wa hospitali 67 za wilaya, fedha hizo zisaidie katika uendeshaji wa viwanda vya ndani na kuongeza fursa ya ajira kwa watanzania.

Waziri Jaffo amerudia kutoa maelekezo hayo baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kituo cha afya Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, unaojengwa na jeshi la kujenga taifa kupitia shirika lake la uzalishaji mali Suma JKT kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 800 ambazo ni sehemu ya michango ya rambirambi kutokana na ajali ya kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea septemba 20 mwaka huu na kusababisha zaidi ya watu 230 kupoteza maisha na wengine 41 kunusurika kifo.

Katika hatua nyingine, mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cornel Magembe amemuomba waziri wa TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo kuangalia uwezekano wa kuwajengea mabweni wanafunzi zaidi ya 1300 wanaoishi kwenye visiwa 25 kati ya visiwa 38 vinavyounda wilaya hiyo, ambao kila siku wanalazimika kusafiri kwa Mitumbwi asubuhi na jioni kwenda mahali zilizojengwa shule za sekondari kuhudhuria masomo.